Oktoba 5, 2020

Elimu Ya Mtandao Kuchochea Mfumo Mseto Wa Kujifunza Katika Elimu Ya Afrika

by Jens Ischebeck

Siku hizi wasomi na wanafunzi katika ngazi mbalimbali za elimu wanajifunza kupitia mtandao. Kumekuwa na mijadala mingi juu ya kuimarisha mafunzo kwa njia ya mtandao pamoja na kuboresha mifumo ya elimu kwa ujumla.


Katika Makala hii, nitaelezea namna ambavyo mfumo mseto wa kujifunza (blended learning) unafanya kazi na jinsi gani utasaidia bara la Afrika kielimu na maendeleo kiujumla. Pia nitaonyesha mikakati madhubuti ya kutekeleza elimu ya masafa (distance learning) barani Afrika.


Makala hii ni muhimu kwa kila mdau wa elimu ya kiteknolojia (EdTech). Pia ina manufaa kwa mwalimu pamoja na mwanafunzi. Vile vile makala hii itamsaidia yeyote mwenye nia ya kuanzisha kampuni ama biashara ya elimu ya kiteknolojia barani Afrika.

Hali Ya Elimu Barani Afrika: Tupo Hatua Ipi?

Ninatambua vyema juhudi za kuleta mabadiliko katika elimu, ikiwemo kuboresha miundombinu inayofanikisha zoezi zima la ufundishaji kivitendo na nadharia.


Sababu kubwa inayopelekea umuhimu wa kubadili au kuboresha mifumo ya elimu barani Afrika ni kwamba, nguvu kazi kubwa ya bara hili ni vijana amabao wengi hukumbana na changanmoto nyingi katika kupata elimu.


Utafiti uliofanywa na shirika la umoja wa mataifa unaonyesha, Afrika ni bara changa likiwa na idadi ya watu milioni 200 huku wengi wao wakiwa ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 34.


Ripoti hiyo inaendelea kusema kuwa rika hili la vijana barani Afrika linaweza kuwa chanzo cha fursa nyingi. Wakipata mwanzo mzuri wa elimu, vijana hawa waweza kuja kuwa wataalamu wa baadae katika fani mbalimbali kama vile udaktari, uinjinia pamoja na fani zingine.


Hata hivyo, mchango wa vijana katkika kukuza uchumi wa Afrika umekuwa mdogo kutokana na vijana hawa kukosa ajira na fursa za kujiendeleza kielimu. Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaendele kusema, vijana wengi wnakumbana na changamoto za kifamilia. Mabinti wengi hulazimika kukatiza masomo ili waolewe au kubaki nyumbani kulea familia.


Wimbi la shida wazipatazo vijana barani Afrika limepelekea baadhi yao kuingia katika maisha hatarishi. Kwa mfano, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, vijana wengi wamejiunga na makundi ya waasi kutokana na kukosa fursa za kupata elimu bora.


Changamoto nyingine ya mfumo wa elimu wa sasa barani Afrika ni kukosekana kwa miundombinu imara ambapo bado kuna maeneo wanafunzi hutembea umbali mrefu kwenda shule.


Pamoja na baadhi ya vyuo vya Afrika kuwa mionngoni mwa vyuo bora duniani kama vile Chuo cha Cape Town nchini Africa Kusini na Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, bado maeneo mengi Afrika hayana vyuo bora. Kwan mfano, nchini Niger kuna chuo kimoja pekee kinachotegemewa kuelimisha maelfu ya wasomi nchini humo.


Hata kwenye nchi tajiri kama Afrika Kusini, shule nyingi zinakosa miundombinu ya kuweza kutekeleza vyema sera za elimu za taifa hilo. Hali ni mbaya zaidi kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara, hasa maeneo ya vijijini ambako watoto wengi hutembea umbali mrefu kufika eneo la shule.


Lakini kwa upande mwingine, bara la Afrika linakuja kwa kasi katika matumizi ya internet. Huwa nawashangaza wasomaji wangu nikiwaambia kwamba, hata kwenye maeneo masikini zaidi Afrika, asilimia 70% ya watu wanamiliki simu. Kwa ujumla, jamii ya watu wa kusini mwa jangwa la sahara inatazamiwa kuwa na upatikanaji wa huduma za intaneti kuliko huduma za chakula bora au maji safi.


Vile vile vijana wengi Afrika wanajihusisha na ujasiriamali ikiwemo kutengeneza na kupakua applikesheni za simu. Hata hivyo, ukilinaganisha na takwimu za upakuaji wa aplikesheni za simu duniani, bara la Afrika bado lina fursa kubwa katika sekta hii.


Kwa sasa, nchi za Afrika kusini, Kenya, Nigeria na Ghana ndizo zinaongoza kuwa na idadi kubwa ya upakuaji wa aplikesheni za simu. Changamoto iliyopo ni kuchochea idadi hii iweze kufikiwa kwa nchi za kusini mwa jangwa ka sahara.


Takwimu zote hizi zina ashiria kuwa elimu ya masafa (Distance Learning) ndiyo chaguo sahihi kwa afrika. Mfumo wa elimu ya masafa ukitekelezwa vyema, utaongeza faida za kimuundombinu na kuweza kutoa fursa ya ekimu kwa vijana wengi.


Hili pia litafungua fursa kwa watu wazima waliokosa elimu ya msingi na sekondari kuweza kujifunza. Utekeleza wa mifumo kama MOOC (Massive Open Online Courses) utaweza kuwa msaada mkubwa.

Mfumo Mseto wa Kujifunza (Blended Learning), Nini Maana Yake Hasa?

Blended Learning, au elimu mseto ni mfumo unaojumuisha njia za kawaida za kujifunza (ana kwa ana) pamoja na zile za kujifunza mtandaoni. Ni mseto wa ‘online’ na ‘offline’ katika kujifunza.


Mafano mzuri wa elimu mseto ni pale ambapo chuo kinaweka masomo mubashara (livestream) na wanafunzi wanaweza kujifunza wakiwa popote.  Shule ya Biashara Mkondoni (Online Business School) ni mfano wa njia hii. Mfano mwingine wa elimu mseto ni ule unaojmuisha kusoma ukiwa mbali kwa kutumia vyenzo zilizopo mtandaoni na zile zisizo mtandaoni. Hapa wanafunzi wanaruhissiwa kukusanya taarifa mtandaoni na kutuma kazi zao na wanapoke mrejesho kwa njia ya posta.


Hii ni baadhi tu ya mifano inayoonyesha jinsi gani njia mbalimbali za elimu zinaweza kuchanganywa na kufanywa kuwa mseto. Jambo la kuzingatia unapotekeleza mfumo mseto wa usomaji ni kuhakikisha inaendana na hali na mazingira ya mlengwa. Kwa mfano, mfumo wa kujifunza kwa njia ya video si muhimu kwa wanagunzi wanaokaa chuoni (campus) hasa ikiwa miundombinu yote inatolewa na serikali.


Kuna hoja zinasema kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao inaweza kushusha motisha ya wanafunzi ambao wangependa kujifunza kwa kutumia nyenzo za darasani. Lakini utoaji mafunzo kwa njia ya mtandao unafaa zaidi kwa wanafunzi walio mbali na chuo.

Taswira Ya Taasisi za Elimu Katika Nchi Za Afrika

Kuna tofauti kubwa juu ya hali za halisi za shule na vyuo mbalimbali kutoka nchi hadi nchi barani Afrika.


Tuchukulie mfano wa chuo kikuu cha nairobi ambapo wanafunzi wanaweza kujifunza kupitia njia za mtandao na za kawaida. Huu ni mfano tu wa taasisi ya elimu ya juu yenye nyenzo za TEHAMA, huduma za afya, maeneo ya michezo pamoja na maeneo ya kufanyia mitihani.


Lakini ni hapa hapa Kenya ambapo shule nyingi hazina mfumo wa kutoa elimu kiteknolojia (Edtech). Hali hii pia ni dhahiri katika Rasi ya Cape nchini Afrika Kusini ambako shule za msingi na sekondari hazina vyoo bora pamoja na vifaa muhimu vya kujifunzia.


Mwalimu mmoja barani Afrika hufundisha darasa lenye idadi ya wanafunzi zaidi ya 90. Hali hii inaonyesha umuhimu wa kuwezesha elimu ya masafa na kuimarisha nyenzo za kidigitali za kujifunzia ili kuwapunguzia mzigo walimu na kuwapa wanafunzi uhuru wa kujifunza bila bughudha ya kubanana darasani.

Kipi Kinahitajika Kufanikisha Elimu Mseto (Blended Learning)

Jibu la swali hili, lafuata majadiliano ya angavu kama ilivyo hapo juu. Kwa ujifunzaji uliochanganywa kuwa na athari nzuri na inayofaa kwa wanafunzi wa Kiafrika, kuna haja ya mtaala na walimu waliofunzwa vizuri kutoa masomo yenye maana na vile vile mikakati ya ujifunzaji wa dijitali ambayo imeundwa kutoshea mahitaji ya darasa la mtu na mwanafunzi.


Hasa, nyanja za dijitali za mkakati wa elimu uliochanganywa zinapaswa kuelekezwa kufikia mapungufu yeyote katika utoaji wa ujifunzaji wa nje ya mkondo katika kituo chochote. Mikakati ya ujifunzaji wa kidijitali inapaswa kuwa kabambe, kuthibitishwa baadaye, kufikiria mbele na iliyoundwa kuwapa wanafunzi elimu bora zaidi bila kujali hali zao za kifedha.


Nicolas Goldstein, mwanzilishi mwenza wa talenteum.africa, anasema: "Kwa ufahamu wangu, lazima niseme kwamba tunahitaji kuchanganya elimu ya mbali na elimu ya ana kwa ana ili kufaulu. Hii ni muhimu kuwa na mtu mbele yako na kuzungumza kuona ikiwa kile ulichojifunza mkondoni kinaeleweka vizuri.


Juu ya elimu rasmi, elimu ya masafa inakupa fursa ya kujifunza haraka utaalam na kila wakati uwe na habari juu ya uboreshaji wa ujuzi. Katika Talenteum.Africa tunapenda kufanya kazi na Talanta ambazo huwa zinafundisha mkondoni na kuwasiliana na ustadi wa habari. Zaidi wewe ni mjanja wa dijitali bora!"


Na Mpumalanga Zwane wa Chuo Kikuu cha Uongozi cha Afrika asema: "Ninahisi mabadiliko ya ujifunzaji mchanganyiko ni fursa nzuri ya kusaidia kukuza Bara mbele. Inaweza kufanya elimu ipatikane zaidi wakati ikiunganisha vizuri sekta hiyo na mwelekeo ambao ulimwengu unasonga.


Walakini, jinsi Bara linavyotumia fursa hii vizuri inategemea juhudi za pamoja za sekta za umma na za kibinafsi ili kufanya muunganisho mzuri wa mtandao upatikane zaidi kwa tabaka zote za kijamii."

Muhtasari: kwa nini mchanganyiko wa kozi za mkondoni na miundombinu ya jadi ya elimu ina faida katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara?

Ili mfumo wa elimu mseto uweze kuleta manufaa kwa wanafunzi wa Afrika, kuna haja ya kuwepo mitaala na wakufunzi mahiri pamoja na mikakati ya kujifunza kidigitali iliyoboreshwa. Yote haya yanapaswa kuandaliwa katika namna ambayo inakidhi mahitaji ya mlengwa.


Ni vyema mikakati ya kujifunza kidigitali ikaandaliwa kuziba mapungufu yaliyopo katika mfumo wa kawaida. Mikakati hii iandaliwe kuendana na mahitaji ya sasa na baadae. Pia impatie mwanafunzi elimu broa bila kujali hali yake kiuchumi.

Muhtasari: Kwanini Mseto Miundombinu ya Kozi za Mtandaoni na Elimu ya Kawaida una Manufaa Kusini mwa Jangwa la Sahara?

Eneo la kusini mwa jangwa la sahara ni eneo muhimu hasa linapokuja swala la kuanzisha utekelezaji wa elimu mseto. Hili ndilo eneo ambalo kuna umasikini mkubwa, miundombinu ya elimu bado ni duni.

Kwa hivyo, mikakati ya maendeleo ya MOOC, e-learning na m-learning inaweza kutarajiwa kutoa faida kubwa zaidi na mabadiliko mazuri.

Kwa jumla, njia iliyochanganywa ya elimu itafaidi sana maeneo masikini ya Afrika kwa sababu ita:

  • Kuboresha miundombinu duni ya elimu
  • Kuondoa changamoto ya miundombinu duni ya usafiri
  • Kuwapunguzia walimu mzigo wa kufundisha madarasa ya wanafunzi wengi
  • Kuwapa wanafunzi fursa ya kupata elimu kutoka vyuo bunifu na wakufunzi kutoka sehemu mbali mbali duniani
  • Kuzipa nguvu jamii masikini
  • Kuwavutia vijana kujifunza na kuwaepusha kuingia katika tabia hatarishi kama kujiunga na uasi.
  • Kufungua fursa za kujiendeleza kitaaluma katika kiwango cha kimataifa.
  • Kuwawezesha watu wazima waliokosa elimu kupata fursa ya kujifunza.
  • Kusaidia kukua kwa ujasiriamali Afrika.

Furaha na Manufaa ya Elimu Mseto

Mfumo ya kujifunza kidigitali na ule wa ana kwa ana vikiweza kuchanganywa vyema, vitaweza kuleta suluhu madhubuti kwa waelimishaji na wanafunzi barani africa.

Kama tulivyoona, ujifunzaji wa kielektroniki hufanya mafanikio ya ujifunzaji mchanganyiko na inapaswa kuwa sehemu muhimu ya mpango wowote wa elimu uliochanganywa.

Toa maoni juu ya makala hii. Pia washirikishe marafiki zako.


Tags


You may also like

Leave a Repl​​​​​y

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

{"email":"Email address invalid","url":"Website address invalid","required":"Required field missing"}