Disemba 12, 2020

Mwongozo Kamili Juu Ya Elimu Kwa Njia Ya Mtandao Afrika

by Jens Ischebeck

Elimu kupitia njia ya mtandao (e-learning) barani afrika sasa ni ndoto inayotimia.

Kukua kwa upatikanaji wa mtandao wa intaneti kumeongeza fursa za kujifunza kupitia kwa kupitia mtandao.

Teknolojia kama vile kusoma kozi mtandaoni (online course) kunaiweka afrika kayika nafasi nzuri katika suala la utoaji elimu kupitia njia nyingi tofauti za kidigitali. Kupitia teknolojia hii, elimu imeweza kufikishwa katika maeneo ,mbalimbali hasa vijijini ambako miundominu bado haijawa imara.

Makala hii, kwa kutumia mifano, inakupa mtazamo wa kina juu ya jinsi gani upatikanaji wa intaneti unaiboresha Afrika. Pia Makala hii inatoa Maoni ya juu ya namna ya kutumia fursa ya upatikanaji wa mtandao wa intaneti katika kuboresha elimu barani Afrika.

Naomba twende sambamba kwenye makala hii.

Mapinduzi ya Elimu Teknolojia (Edtech)

Kutokana na tafsiri ya Shirikisho la Teknolojia ya Elimu Mawasiliano, elimu ya kiteknolojia (Edtech) inatafsiriwa kama "taaluma ianyowezesha utendaji kwa kuunda, kutumia na kusimamia michakato na rasilimali sahihi za kiteknolojia."

Elimu ya kiteknolojia (Edtech) inajumuisha vifaa vya kiteknolojia vinavyohitajika katika kujifunza Pamoja na nadharia itumikayo kuboresha matoke ya elimu inayotolewa.

Katika miaka ya hivi karibuni, matumizi ya teknolojia ya kuwezesha kujifunza yameongezeka sana duniani kote. Waelimishaji wanaweza kupata zana kama zile za kujifunza ki-elektroniki, kozi za mtandaoni, Pamoja na mfunzo ya kutumia video, picha au sauti (media) ili kuwapa wanafunzi upatikanaji wa taarifa.

Nini maana ya kujifunza kimtandao?

Neno kujifunza ki-elekronoki (e-learning) limekuwa likitumika tangu miaka ya 1990 ambapo lina maanisha – matumizi ya vifaa vya kielektroniki katika mazingira ya kujifunza. Inaweza kuwa kozi za mtandaoni, kufundisha kwa kutmia picha na video za kidigitali Pamoja na mifumo mingine ya kidigitali.

Njia ya kujifunza kwa kupitia mtandao imeendelea kubadilika kadri miaka ipitavyo. Kwa sasa ‘e-learning’ imepata maneno mapya kama vile ‘mobile learning au m-learning’ ambayo yanamaanisha kujifunza kwa njia ya simu za mkononi, tableti Pamoja na kompyuta mpakato.

Hili linajidhihirisha barani Afrika ambapo kutokana na shirika la UNESCO, Watoto takribani milioni 30 wenye umri wa kwenda shule za awali wanashindwa kwenda shule kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa ada, kuacha shule, magonjwa mlipuko Pamoja na kukosa motisha ya kwenda shule.

Mwenendo wa hivi karibuni umeshuhudia kuanzishwa kwa kozi za mtandaoni kwa wingi (MOOC). Nyingi zikiwa za bure na nyingine za kulipia. Usomaji huu wa kimtandao unatazamiwa kuondoa pengo lililopo kwenye upatikanaji wa elimu katika jamii zisizofikiwa.

Pamoja na faida zake nyingi, mfumo wa MOOC pia unatoa majukwaa ya kujifunza yenye ushiriki wa wanafunzi na waelimishaji.

Nani Mnufaika wa Elimu ya Ki-mtandao?

Kujifunza kwa njia ya mtandao ni raslimali adhimu ambayo inaongeza tija Zaidi ukilinganisha na mazingira ya kawaida ya kijifunza na kufundisha.

Njia hii inaweza kuwa mkakati wa kuwasilisha maarifa kama vile kozi za vyuoni, kutoa msaada darasani, Pamoja na kuimarisha maendeleo ya kitaaluma kwa wafanyakazi.

Fursa Gani Zinapatikana kwa Wanaojifunza Kupitia Mtandao?

Afrika ipo kwenye wakati muafaka wa kufurahia matunda yatokanayo na kukua kwa elimu ipatikanayo kimtandao. Hii inatokana na kukua kwa matumizi ya simu huku upatikanaji wa intaneti pamoja na teknolojia zingine ukiwa ukiendelea kuimarika.

Jambo muhimu kutambua ni kwamba, idadi kubwa ya watumiaji wa mtandao wa intaneti wanatumia simu za mkononi. Hii inatokana na ukweli kwamba kupata intaneti kupitia sim uni rahisi ukilinganisha na njia nyingine kama kompyuta za mezani (desktop).

Kwa kuwa watu wana miliki simu janja kwa wingi, changamoto imebaki ni jinsi gani Afrika inaweza kutumia hii fursa kama nyenzo ya kufanya elimu inamfikia kila mmoja.

Upatikanaji wa intaneti barani afrika unatofautiana kutoka nchi mmoj hadi nchi nyingine. Kuna baadhi ya nchi kusini mwa jangwa la sahara ambako idadi ya wanaotumia intaneti hata haifikii nusu ya idadi ya watu.

Wacha tutazame takwimu ili kupata uhalisia wa upatikanaji wa intaneti Afrika. Data hizi ni taarifa ya hadi mwezi Machi, 2020.

 • Kenya: 87%
 • Nigeria: 61%
 • South Africa: 55%
 • Ghana: 38%
 • Ethiopia: 17%

Kutokana na data hizi, ni Dhahiri kwamba upatikanaji wa intaneti katka bara la Afrika unatofautiana kutoka nchi moja hadi nchi nyingine. Hivyo, hata utoaji wa elimu kiteknolojia (edtech) ni lazima uzingatie hili ili kuzingatia idadi ya watu katika eneo husika.

Hata hivyo, jambo la kutia matumaini ni kwamba, huduma nafuu za upatikanaji wa intaneti zinazidi kuimarika.

Takwimu za hivi karibuni za kampuni ya GSMA zinaonyesha kuwa, upatikanaji wa intaneti unaendelea kupanda.Kutokana na Maoni ya watumiaji wa mtandao, kuna changamoto kubwa mbili katika upatikanaji wa mtandao intaneti kusini mwa jangwa la sahara ambazo ni; kukosa maarifa na elimu ya kidigitali ikifuatiwa na gharama kubwa za kupata intaneti

Mtandao wa Forbes, unaitaja Afrika kama sehemu inayokuja juu kwa matumizi ya intaneti.

Kuna umuhimu mkubwa kutafakari faida na hasara za mu kusoma kupitia mtandao. Hii itasaidia kukabiliana na changamoto zinazotikana na zoezi zima la kujifunza kupitia mtandao, na kwamba utaweza kubuni mbinu za kulifanya zoezi liwe bora.


Faida za Kujifunza Ki-mtandao

Kozi za mtandaoni zina faida kubwa sana endapo msomaji atakuwa na motisha ya kujifunza. Faida hizi zinategemea hamasa na uatayari wa mtu binafsi.

Faida hizi zinaweza kuwekwa kwenye makundi matatu ambayoo ni; urahisi wake, unafuu wa gharama, na uharaka w kufikika.

Tazama faida zaidi hapa chini:

 • Kozi za mtandaoni zinapatikana na kufikika kirahisi
 • Zinaokoa gharama
 • Zinatumia teknolojia ya kisasa
 • Hakuna ubaguzi (kila mtu anaweza kusoma kupitia mtandao)
 • Wanafunzi wenye asili ya upweke inawafaa sana
 • Ushirikiano mkubwa kati wa wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali duniani
 • Ushirikiano mkubwa kati ya Mwalimu na wanafunzi.

Hasara za Kusoma Kidigitali

Kama mwanafunzi hajitambui, na hana msukumo binafsi, njia hii ya kujifunza haitamsaidia. Ukiondoa kutokuwepo utayari wa mwanafunzi, changamoto nyingine ni kama ifuatavyo;

 • Gharama za kutumia teknolojia
 • Inamzuia msomaji kuwa na maingiliano na watu wanomzunguka
 • Inagharimu muda wa kupanga ratiba.

Sasa wacha tutazame hali ya usomaji wa ki-mtandao ilivyo nchini Ghana pamoja na Afrika Kusini.


Utafiti ulifanywa hivi karibuni na bwana Marfo pamoja na Okina (2010) unaonyesha asilimia 98.35 ya watu katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Kwame Nkrumah (KNUST) walikubali kwamba usomaji kuptia mtandao utaboresha namna yao ya kujifunza.

Hu uni mfano mzuri kutoka KNUST, kwani unaonyesha jinsi gani ‘e-learning’ inaweza kutumika kuboresha mazingira ya kusoma.

Jukwaa la ki-mtandao, Moodle, lilitumika kuandaa nyenzo za kufundishia darasani na vile vile kuwaandaa walimu juu ya jinsi ya kutuma matangazo na email za jumla kwa wanafunzi.

Wakati huohuo, mipango bado ianaendelea  kuwezesha utoaji wa wa kozi kwa njia ya masafa (remote learning). Hii itawasaidia kwa kiasi kikubwa wanafunzi wanaokwamishwa na miundombinu duni. Vilevile mipango hii itawezesha wanafunzi wenye uwezo tofauti hasa wale wenye ulemavu ambao mara nyingi husahaulika inapojengwa miundombinu mipya.

Mfano mwingine wa elimu ya kiteknolojia ni ule kule nchini Nigeria ambapo usomaji wa stashahada za lugha hufanywa kupitia mtandao. Wanafunzi husoma kupitia simu zao, hufanya majaribio pamoja na kupatiwa cheti.

Kuna idadi kubwa ya watoa elimu kupitia mtandao nchini Afrika Kusini ikijumuisha shule, vyuo, asasi kiraia na makampuni binafsi.

Vyuo mashuhuri kama Chuo cha Cape Town, Chuo cha Stellenbosch, pamoja na kile cha Wits hutoa kozi za mtandaoni kupitia mfumo wa MOOC. Kozi hizi zimeandaliwa kukidhi mahitaji ya kiafrika.

Mfano mzuri ni chuo cha MOOC SA mabacho kinatoa kozi bure mtandaoni. Chuo hiki hutoa kozi mbalimbali kutoka wataalamu tofauti chini humo. Malengo ya chuo hiki ni kufikisha elimu bure kwa wenye uhitaji. Hakijali swala ya kutunuku ubobeaji.

Mchango wa serikali katika maendeleo ya kusoma kupitia mtandao unaonekana kupitia Idara ya Elimu ya Cape Town ambayo imeunda mkaktai uitwao ‘Game Changer Strategy’. Sehemu ya mkakati hu uni kuunda jukwaa la mtandaoni (e-portal) ambapo wanafunzi pamoja na walimu wanaweza kupata taarifa na nyenzo za kidigitali kama vile aplikesheni za simu, vibatu pepe, video na kozi za mtandaoni.

Mfano mwingine wa kuvutia ni pale ambapo THINK Digital College ilianzishwa mnamo mwaka 2016 ili kutoa elimu mbadala kwa Watoto ambayo ina gharama nafuu na inapatikana kwa urahisi kwa kutumia simu iliyounganishwa na intaneti.

Kuna idadi kubwa ya watoaji wa elimu ya mtandaoni barani Afrika. Baadhi yao wamejikita katika elimu ya awali huku wengine wamelenga elimu ya juu. Kwa kutaja baadhi, wafuatao ni watoa elimu kupitia mtandao maarufu Afrika.


Eneza ni moja kati ya jukwaa la kutoa elimu ya mtandao linalotumiwa na wengi Afrika. Lilianza na mfumo wa jumbe fupi za meseji, sasa lina tovuti na aplikesheni ya simu.


Rethink Education (South Africa):

Hili ni jukwaa na kidigitali linalotumia mfumo wa kutumiana meseji fupi, masomo shirikishi hasa masomo ya hisabati na sayansi.


Prepclass.com (Nigeria):

Hili linatoa mafunzo kuhusu mitihani ya ndani. Hutoa mbinu za kujibu mitihani kulingana na somo au mada. Majaribio hutolewa kwa mfumo wa kompyuta (Computer Based CBT) ikiwa ni saw ana ule UTM (Unified Tertiary Matriculation Examination).


Jukwaa hili linatoa kozi za mtandaoni kupitia simu za mkononi. Upatikanaji wa kozi hizi ule wa mtandaoni (online) pamoja na ule wa kawaida (offline).


Ubongo (Tanzania):

Ubongo hutoa elimu inayolenga kuwapa maarifa Watoto kwa gharama nafuu kupitia katuni.


Ecampus.camp (Ghana):

Jukwaa hili hutoa maandalizi mahsusi ya mitihani, majaribio kupitia mfumo rafiki ambapo mtumiaji anaweza kuendelea kwa wakati wake.


Kuna idadi kubwa ya watoa elimu kwa njia ya mtandao duniani. Idadi hii inaendelea kukua kwa kasi. Nataka nikudokeze juu ya watoa elimu ki-mtandao maarufu duniani.

Udemy

Udemy ni jukwaa maarufu duniani linalotoa aina mbalimbali ya kozi mtandaoni. Faida kubwa ya jukwaa hili ni kwamba lipo kimataifa Zaidi kwani kozi zake hutolewa katika lugha Zaidi ya 80.

Coursera

Coursera ni jukwaa linaloongoza kutoa kozi mbalimbali kutoka vyuo marufu duniani. Jukwaa hili hutoa soko kwa waelimishaji mbalimbali duniani kuweza kuweka mafunzo yao.

Online Business School

Online Business School hutoa koi zilizo thibitishwa kwa ngazi ya shahada. Unaweza kupata shahada kupitia kusoma mtandaoni (online)

Bill Gates aliwahi kuandika katika barua yake ya 2015 kupitia Bill Melinda Gates Foundation kwamba, “tunakoelekea elimu yenye kiwango cha kimataifa itakuwa inapatikana viganjani mwetu”

Habari njema ni kwamba elimu ya mtandaoni inaweza kuondoa changamoto za umbali na kuweza kuondoa pengo ili kuhakikisha kila mtu anapata elimu bora. Kama tunavyoshuhudia, sasa watu wanaweza kupata shahada kama vile MBA kupitia mtandao endapo chuo anachosomea kimepewa kibali cha kutunuku cheti na kina vyenzo za kutosha.

Kwa mfano, chuo cha tofali na chokaa nchini Marekani kinaweza kutoa program za mafunzo katika eneo la shule lakini pia kikatoa mafunzo hayo mtandaoni. Ingawa yale ya mtandaoni hayatahusisha majaribio halisi (practical). Vile vile msomji wa kupitia mtandaoni  hana ulazima wa kuhudhuria masomo kwa muda uliopangwa darasani.

Mkurugenzi wa Mtandao wa Shule ya Biashara za Kimataifa ambaye pia ni mwana uchumi ndugu Guy Pfeffeerman anagusia jinsi Afrika inavyoweza kufikia Malengo ya Kimataifa ya Milenia yam waka 2000. Anasema njia pekee ya kufikia malengo ya elimu barani Afrika ni kupitia mfumo wa kujinza kwa njia ya mtandao ili kupata program kama vile MBA na shahada za awali katika fani mbalimbali. Mfumo huu wa kujifunza mtandaoni utasaidia Afrika kukuza uchumi wake.

Ingawa neno mtandaoni (online) lilianza kutajwa takribani miaka 30 iliyopita, sasa limechukua sura mpya. Karne ya 21 imeleta teknolojia za kisasa. Intaneti na kompyuta zinapatikana kote afrika.

Hapa mfano wetu wa chuo cha tofali na chokaa kutoka nchini Marekani ambacho pamoja na mafunzo ya shuleni, vile vile kinatoa elimu kupitia mtandao unafaa zaidi.

Miaka michache iliyopita, afrika ilipokea mkonga wa mawasiliano kwa mara ya kwanza. Tangu hapo kumekuwa na mikonga ya mawasiliano kwa wingi inayopatikana katika Pwani za afrika mashariki na magharibi. Kila mwaka nchi nyingi Zaidi afrika zinazidi kuunganishwa na intaneti.

Uwepo wa elimu ya kiteknolojia Afrika unaashria fursa kwa Vijana wenye kiu ya kutafuta maarifa. Ingawa bado kuna changamoto nyingi zinazoikabili elimu ya Afrika, mambo kama vile kikwazo cha lugha, gharama n.k. – bado ni kikwazo. Lakini teknolojia inatarajiwa kutatua tatizo hili.

Teknolojia inaweza kutoa nyenzo bora za kujifunzia ambazo zinapatikana kwa kila mwanafunzi. Hili likifanikiwa, usawa wa elimu barani Afrika utafikiwa.

HITIMISHO..

Elimu ya kiteknolojia (edtech), kozi za mtandao pamoja na mabo mengine yanayohusisha teknojia katika kujifunza na kufundisha inaweza kutumika katika namna tofauti. Wadau wengi walitazama hili kama njia ya kupunguza ujinga miongoni mwa watu.

Hata hivyo, uwepo wa umeme imara pamoja na upatikanaji wa intaneti ya kasi vinahitajika kuweza kufikisha mafunzo haya kwa walengwa. Pia mifumo hii italeta ufanisi Zaidi ikienda sambamba na ile mifumo iliyopo ya ufundishaji mashuleni.

Kama tulivyoona kwenye mfano wetu wa chuo cha Ghana (KNUST), walimu na wanafunzi wameona ufanisi wa majukwaa ya kimtandao ya kujifunza kama vile Moodle. Mifumo kama hii inaweza kutumiw sambamba na vifaa vingine vya kiteknojia kuleta mafanikio bora ya baadaye Afrika.

Kwa kumalizia, baadhi ya kozi za mtandaoni zinaweza kuwa chachu ya kuleta mapinduzi ya elimu kwa waafrika. Kozi hizi zitawezesha watu kujifunza maarifa mapya, ama kuiendeleza na kuweza kutunukiwa shahada kama vile MBA, na shahada zingine katika taaluma mbalimbali. Hili litaweza kuboresha Maisha ya watu na kuwawezesha kuwa wajasiliamali wa kimtandao.

Kwa ujumla, ongezeko la kozi za mtandaoni pamoja na upatikanaji wa intaneti unaiweka afrika katika nafasi nzuri ya kunufaika kiuchumi kwa watu wa jinsia zote. Aina hii ya usomaji inampa mtu uhuru wa kusoma akiwa anaendele na shughuli zake za nyumbani au majukumu kazini.

Tofauti na nchi za ulaya, jamii za afrika zinaishi kwa ukaribu yani kuishi kindugu, na kifamilia. Wakati mwingine hili huleta kikwazo pale inapofikia mtu anaenda kusoma mbali na kuacha majukumu ya familia. Hivyo usomaji wa mtandaoni utaleta suluhu thabiti.

Ni matumaini yangu kuwa umefurahia Makala hii kuhusu usomaji wa kupitia mtandao katika afrika. Kama umewahi kusoma kozi yoyote mtandaoni, ningependa kusikia uzoefu wako.


Toa Maoni yako kwenye uwanja wa kutolea maoni (comment).


Tags


You may also like

Leave a Repl​​​​​y

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

 1. Nimeisoma makala hii kwa mapana yake na nishukuru kuwa imeeleza kwa kina namna Tanzania ?? na Africa kwa ujumla imepiga hatua katika matumizi ya Intaneti katika kujifunza. Suala la msingi hapa ni kuwa bado tuna njia ndefu ya kutembea kufikia mafanikio kama yalivyo Mataifa mengine ya Ulimwengu wa Kwanza. Nasema hivyo kwani leo tunavyoongea umma mkubwa wa Watanzania hawana mlo ata mmoja achilia nyenzo kama umeme ambayo ni sawa na mbingu na ardhi, havikutani!

{"email":"Email address invalid","url":"Website address invalid","required":"Required field missing"}