Novemba 16, 2020

Jinsi Ya Kukabiliana na Changamoto 3 za Ukosefu wa Usawa Katika Upatikanaji wa Elimu Africa.

by Jens Ischebeck

Ukuaji wa idadi ya watu dhidi ya Mahitaji ya Kielimu Barani Afrika

Ukosefu wa usawa wa kielimu ni swala dhahiri barani Afrika. Kuna watoto zaidi ya milioni 128 wenye umri wa kwenda shule katika Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara. Lakini watoto milioni 17 wako kwenye hatari ya kutoliona darasa.

Ukweli mwingine ni huu; Watoto milioni 37 wa Kiafrika wanapata nafasi ya kuhudhuria shule, lakini kile wanachojifunza hakiwapi mwendo mzuri katika uchumi wa leo.

Sababu kama kuwepo kwa na umaskini, idadi kubwa ya watu, vikwazo vya lugha na tawala mbovu, ndio chanzo cha wanafunzi wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kuwa na shida kupata kiwango cha elimu bora iliyoandaliwa kwa manufaa ya wote.

Ikiwa wewe ni mwanafunzi, mwalimu au mtaalamu wa elimu barani Afrika - bila shaka una mtazamo chanya juu kozi za mtandaoni - ujifunzaji wa rununu (m-learning) na kujifunza kwa njia ya elektroniki juu ya jinsi gani vifaa hivi vina nguvu kuandaa mustakabali mzuri wa Afrika.

Hiyo ni moja ya sababu za kukuza elimu ya masafa na kuongeza usawa katika elimu kwa wanafunzi wa Jangwa la Sahara.

Je! Ni Nini Taswira ya "Upataji wa Elimu Barani Afrika"?

Upatikanaji thabiti wa elimu barani Afrika unategemea mambo kadhaa.

Hizi ni sababu za kupunguza hali ya kutokuwa na usawa wa elimu:


• Eneo la kijiografia la shule

Mahali ambapo shule ziko inategemea mambo anuwai. Baadhi ya maeneo barani Afrika yana watu wengi, na mengine hayana. Kigezo cha wingi wa watu hupelekea maamuzi ya serikali kujenga shule. Hivyo, maeneo yenye watu wachache hujikuta hayana shule au shule iko mbali.


Uwiano wa Idadi ya Shule na Umbali

Idadi ya shule zinazopatikana kwa kila mkoa na umbali ambao watoto wanapaswa kusafiri kufika shuleni inapaswa kuzingatiwa. Watoto wanalazimika kusafiri umbali mrefu kufika shuleni kwa masaa yasiyoweza kueleweka na miundombinu duni ya barabara na ukosefu wa usalama katika kaunti zao na jamii.


Hofu ya gharama ya ada ya shule

Je! Ni wazazi wangapi wanaweza kumudu kupeleka watoto wao shule za kulipia? Bila shaka ni wachache. Wengi hukwepa kutoa pesa zao walizizipata kwa tabu kilipia ada na michango mingine ya shule.


Mtazamo wa wazazi na viongozi kuhusu elimu

Je! Ni wazazi na viongozi wangapi wanaotambua elimu kama haki ya kimsingi kwa wote? Suala hili la tamaduni za kijamii linasimama katika mzizi wa watoto kuachishwa shule. Haki ya watoto ya kupata elimu haithaminiwi.

Zaidi ya asilimia 40% ya watoto katika nchi saba za Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwa ni pamoja na Nigeria, Zambia na Ethiopia hawana stadi za msingi za kujifunza zinazotarajiwa kwa mwanafunzi wa darasa la tano. Kuacha shule katika sekondari na hata kiwango cha msingi ni utaratibu wa kawaida katika sehemu kubwa ya nchi hizi.

Kutokana na ukosefu wa vifaa sahihi vya elimu, nusu ya watoto Kusini mwa Jangwa la Sahara watakua bila kujua kusoma, kuandika, au kuhesabu. Hiyo inasababisha ukosefu wa usawa wa elimu na mapato.


Sasa, ni vipi vikwazo vya kushinda ukosefu wa usawa wa elimu?

Kikwazo cha Ukosefu wa usawa wa Elimu # 1: Mfumo wa Elimu Uliopo barani Afrika

Hata katika mikoa ambayo taasisi za elimu zinaonekana kuwa vizuri, uandikishaji na takwimu za maendeleo hazina si za kuridhisha. Kwa sababu ya ukosefu wa ufundishaji bora na uthabiti wa rasilimali za kufundishia, kuna marudio mengi ya daraja.

Idadi ya watoto wanaofaulu kumaliza elimu ya msingi ni wachache ukilinganisha na idadi ya walioanza. Hali hii inamaanisha shule za msingi zimejaa kuliko shule za upili.

ukizungumzia juu ya wafanyikazi wa kufundisha, walimu wenye uzoefu wa muda mrefu  wanalipwa zaidi kuliko wenzao ambao hawana uzoefu. Maana yake ni kwamba katika shule ambazo wafanyikazi wengi ni wakubwa, takwimu za mishahara ni kubwa.

Hii inasababisha shule kuajiri wafanyikazi wadogo na kuwaacha waalimu wakubwa mapema kuliko  inavyotarajiw. Yote haya yanasababisha ukosefu wa usawa wa elimu inayotolewa katika shule hizi.

Kwa kuzingatia mambo haya yote, mfumo wa sasa wa elimu barani Afrika hauna ufanisi mkubwa lijapo suala la kusaidia vijana kukuza na kuendeleza kazi za maendeleo.

Kikwazo cha Ukosefu wa Usawa wa Elimu # 2: Unafuu wa Elimu

Ingawa shule zingine zinazofadhiliwa na serikali ni bure, wanafunzi katika nchi nyingi za Kiafrika wanapaswa kulipia vifaa vya shule na sare.

Wastani wa elimu ya shule ya upili hugharimu karibu dola mia tano kwa mwaka katika nchi nyingi za Kiafrika. Ni asilimia ndogo tu ya Waafrika ambao wameajiriwa katika tasnia za hali ya juu kama vile madini, kilimo na mafuta na gesi ambapo mishahara iko upande wa juu ndio wanaoweza kumudu elimu bora kwa watoto wao.

Hapo ndipo kuna umuhimu wa watoa huduma ya ujifunzaji wa elektroniki kuzuia kukosekana kwa usawa wa elimu na kuleta ufikiaji wa elimu ya bei rahisi kwa watoto wengi wasio na masomo barani Afrika.

Kikwazo cha Ukosefu wa usawa wa Elimu # 3: Vikwazo vya Lugha

Lugha ya kufundishia imekuwa ni moja ya sababu kuu za wanafunzi kuacha shule kwa wingi. Ukiongezea adha za watoto kusafiri kwa miguu na wakati mwingine kwa basi au gari moshi kufika shuleni, bado pia kuna changamoto ya kitamaduni kwani Afrtika inasifika kwa kuwa la lugha nyingi za kikabila.

Kwa bahati mbaya, ni ngumu kwa watoto kusoma kwa lugha nyingine tofauti na ile yao.

Hii inaweza kuwa uzio mkubwa wa zana za elimu ya kitamaduni kulingana na uchapishaji na masomo ya ana kwa ana. Kwa upande wa elimu ya kiteknoloji (Edtech), changamoto za kilugha zinaweza kupunguzwa kwa msaada wa programu za kutafsiri, zilizowekwa tayari katika bidhaa za ujifunzaji wa elektroniki.

Ukosefu wa usawa wa elimu upo kila mahali.

Lakini hapa kuna ufumbuzi kupitia kujifunza Kielektroniki

Je, Kujifunza Kielektroniki ndio Suluhisho la Mahitaji ya Afrika Leo?

Kujifunza kwa njia ya Elektroniki huleta usawa kwa mapungufu kadhaa ya kitamaduni, kijiografia, kidemografia, na kiuchumi. Mtu yeyote anaweza kujiunga na kozi za mkondoni, umri sio sababu.

Kozi nyingi zinazopatikana mtandaoni  (MOOC) ni kozi za bure za  kwa wale wenye uwezo wa kutumia mtandao (internet). Kozi hizi hazitoi vyeti ama uthibitisho wa kitaaluma, lakini kiwango cha maarifa yanayotolewa unakaribiana na ule utolewao kwenye taasisi za elimu.

Baadhi ya kozi za mtandaoni zilizo maarufu na kupendwa zaidi duniani ni Udemy na Coursera .

African Virtual University (AVU) ujumuisha wanafunzi na vyuo katika nchi zilizoendelea kutoa MOOC. Kuna mashirika mengine kadhaa yanayotoa programu hizi bora.

Pia mafunzo kama haya hutolew vilevile na Online Business School nchini Uingereza. Inatoa kozi kwa wanafunzi kutoka sehemu mbali mbali duninani na kuwapatia vyeti vinavyotambulika duniani.

Habari njema ni kwamba, hata kwa wanafunzi ambao wameshatimiza masomo ya kiwango cha msingi au sekondari tu, bado wanaweza kujifunza na MOOC. Shule na vyuo vikuu hutumia programu maalum ya MOOC kufundisha na kuwasiliana na wanafunzi wao kupitia zana za video kama vile Skype na WhatsApp. Hii ndio huitwa elimu mseto au elimu mchanganyiko.

Walakini:

Je! Mtandao Unapatikanaje Afrika?

Katika sehemu nyingi za Afrika, bado kuna usumbufu wa umeme mara kwa mara na ufikiaji duni wa mtandao.

Wakati ambapo ujifunzaji wa rununu bado unashika kasi, itachukua miaka kadhaa kwa programu za kujifunza kielektroniki kuenea juu ya bara hili. Upande mzuri ni kwamba, hata kwa muunganisho duni wa mkondoni, wavuti imepenya katika kila nchi ya Kiafrika na inaendelea kufanya hivyo kwa mafanikio.

Uunganishaji wa mtandao  na wavuti wa haraka unabaki kuwa kitu cha kufanyiwa kazi na watoa huduma.

Wanafunzi kote Afrika huhamisha pesa kupitia mtandao, wanauwezo wa kuungana na marafiki kupitia mitandao ya kijamii, na kujiunga na mengi ya hivi karibuni ambao yako katika ununuzi mkondoni.

Asilimia kubwa ya Waafrika wanapata mtandao kupitia ‘kompyuta binafsi’ na kompyuta ndogo na katika simu zao mahiri ambapo wanaweza kusoma wanapoendelea na kazi zao.

Hiyo inahamazisha watu kujisajili kwa ujifunzaji wa rununu (m-learning). Hii inasababisha kozi nyingi mtandaoni  kuanza kufuatiliwa na vijana wa Afrika.

Kwa muunganisho wa mtandao wa haraka, kuna kuongezeka kwa idadi ya kampuni za mitaa na za kikanda ambazo hutoa bidhaa na vifaa kwa kozi za mkondoni na maandalizi ya mitihani katika (m-learning).

Mwitikio wa Serikali za Afrika juu ya masomo ya elektroniki

Wanasiasa na viongozi kote Afrika wanatsamani na wana harakia kugundua na kutumia faida zinazo wasilishwa na MOOC Edtech. Nchi kumi na tisa za Kusini mwa Jangwa la Sahara zimejiandikisha na Chuo Kikuu cha African Virtual (AVU) kuanzisha kujifunza kielektroniki kama mkakati wa muda mrefu wa maendeleo ya elimu.

Mbali na mipango ya serikali, kuna kampuni za kibiashara zinazojaza pengo la elimu. Mipango kama programu ya African Leadership University (ALU) ambayo inakusudia kuanzisha mtandao wa vyuo vikuu ili kukuza ujuzi wa uongozi kwa wanafunzi wengi wa Kiafrika kadri iwezekanavyo.

Ukosefu wa Usawa wa Elimu na Mustakabali wa Kujifunza Kielektroniki barani Afrika

Serikali kadhaa zinafanya kazi na nchi katika ulimwengu ulioendelea pamoja na NGOs kuanzisha mitandao ya shule kwenye wavuti sehemu mabalimbali Kusini mwa Jangwa la Sahara. Sera mpya zinazoendeshwa na teknolojia tunazoshuhudia katika nchi za Afrika ziko nyuma ya mradi wa ujifunzaji wa elektroniki.

Mawazo haya yote yana kusudi la kupunguza ukosefu usawa katika elimu barani Afrika.

Hata hivyo, pamoja na sera zilizopo, Afrika inahitaji mchakato ulioboreshwa ili kuhakikisha utunzaji sahihi wa kiufundi wa mitandao ya ujifunzaji wa elektroniki.

Afrika inabidi ichukue hatua zaidi ili ujifunzaji wa kielektroniki upatikane kwa wote, huku ikidumisha na kudumisha uwezo wa ndani. Kwa kufanya hayo, tutaweza kuleta usawa katika upatikanaji wa elimu barani Afrika.

Shiriki nakala hii ndani ya marafiki wako. au niambie tu maoni yako na utoe maoni nakala hiyo!


Tags


You may also like

Leave a Repl​​​​​y

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *

{"email":"Email address invalid","url":"Website address invalid","required":"Required field missing"}